Waziri Wa TAMISEMI, Selemani Jafo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo wamempongeza Balozi wa Utalii nchini, Nangasu Warema kwa namna anavyojitolea kuhamasisha utalii.
Viongozi hao wametoa pongezi hizo walipoungana na baadhi ya wasanii akiwemo Kulwa Kikubwa ‘Dude’ na Amin Mwinyimkuu kutembelea vivutio vinavyopatikana ndani ya Wilaya ya Kisarawe ambapo kabla ya kuanza kwa ziara yao walifika katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo, na baadae waliambatana naye kuelekea kwenye vivutio vya kitalii.
Kwa upande wake balozi huyo amewataka watanzania kumuunga mkono katika kufanya utalii wa ndani kwani yapo mambo mazuri yanayopaswa kuendelezwa hususani kwa vizazi vijavyo, huku akihimiza watu kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vyao ili kukuza sekta ya utalii nchini.