Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Selemani Jafo amebainisha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa Mabweni ya shule za Sekondari Sejeli na Kongwa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Waziri Jafo amesema hayo katika ziara yake wilayani Kongwa ili kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotekelezwa wilayani humo, ambapo amesema fedha za ujenzi wa mabweni ya shule hizo zimetolewa tangu mwezi Januari mwaka huu lakini bado ujenzi huo uko katika hatua za msingi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Omary Mkulo anaeleza sababu za kutokukamilika kwa machinjio hiyo.
Baada ya kufika katika shule ya sekondari Sejeli na kuona hatua ya ujenzi wa bweni la shule hiyo, waziri Jafo anakerwa na hatua ya ujenzi wa bweni hilo.
Waziri Jafo pia ametembelea ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Kongwa ambapo pia hakurizishwa na hatua ya ujenzi ilipofikia.
Hata hivyo Waziri Jafo ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa majengo ya kituo cha afya cha Ugogoni wilayani Kongwa ambayo yanatarajiwa kukamilika hivi karibuni.