Waziri Gwajima azindua Kliniki Tembezi za TB

0
177

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amezindua kliniki tembezi za kisasa nne zikiwemo pikipiki mpya 160, mashine 50 za GeneXpert pamoja na mashine 179 za ECG sentence gharama ya billioni 6.2 ambazo zitarahisisha utoaji huduma Kifua Kikuu (TB) na Ukoma kwa kuwafikia wagonjwa mahali popote kwenye halmashauri nchini.

Dkt. Gwajima amezindua kliniki hizo leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma huku  uzinduzi huo ukihudhuriwa na baadhi ya viongozi ngazi ya Wizara, TAMISEMI na Mkoa lengo likiwa ni kuboresha huduma za matibabu ya ugonjwa wa TB na Ukoma ili kuutokomeza kabisa nchini.

Dkt. Gwajima amesema jumla ya shilingi bilioni 6.2 za kitanzania zimetumika kununua kliniki tembezi na vifaa vya kutolea huduma za afya ikiwemo magonjwa ya TB na Ukoma, huku  akiwapongeza watumishi wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma kwa kufanikisha zoezi hili.

“Nimetaarifiwa kuwa, jumla ya shilingi bilioni 6.2 za kitanzania zimetumika kununua kliniki tembezi na vifaa vya kutolea huduma za afya. Kiasi hiki ni kikubwa, sina budi kuwapongeza watumishi wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma kwa kufanikisha zoezi hili.” Amesema.

Dkt. Gwajima.
amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2020, Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa 135,000, huku kati ya hao waliofanikiwa kubainiwa na kuwekwa kwenye matibabu walikuwa 85,597 sawa na asilimia 63, na kusisitiza kuwa Tanzania  ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye tatizo kubwa la Kifua Kikuu.

Ameongeza kuwa, takribani watu 26,800 wamefariki katika kipindi cha mwaka 2020 licha ya jitihada zinazofanywa na wizara katika kufikia malengo ya kutokomeza Kifua Kikuu nchini, bado nguvu ya ziada inahitajika ili kuweza kuwafikia na kuwaibua wagonjwa takribani 49,403 ambao hatukuweza kuwa naibu na bado wanaendelea kuambukiza ugonjwa huo katika jamii yetu.

“Takribani watu 26,800 walifariki katika kipindi cha mwaka 2020 licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na Wizara katika kufikia malengo ya kutokomeza Kifua Kikuu nchini, bado tunahitaji nguvu ya ziada.