Waziri Aweso: Msiwabambikie wateja Ankara za maji

0
149

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewaagiza Mameneja Masoko wote wa mamlaka za maji safi nchini kusimamia kikamilifu usomaji mita za maji, ili kuepuka kuwabambikia Wananchi bili za maji.

Waziri Aweso ametoa agizo hilo mkoani Mwanza, ambapo amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji kuwasimamia Mameneja Masoko wa Mamlaka za Maji wasiwape wasoma mita za maji malengo makubwa ya makusanyo ambayo hayatekelezeki na yanayowaumiza Wananchi.