Waziri auawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake

0
199

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Kazi na Ajira wa Uganda Kanali Mstaafu Charles Okello Engola ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake.

Polisi nchini Uganda wamethibitisha tukio hilo na kusema kuwa limetokea leo asubuhi katika kitongoji cha Kyanja Kampala, ambako ni nyumbani kwa Waziri huyo.

Kwa sasa polisi wameimarisha ulinzi katika eneo lilipotokea tukio hilo.

Mlinzi anayedaiwa kufanya mauaji hayo naye amejiua na inasemekana kabla ya kufanya mauaji hayo alidai kuchoshwa hali ya kutolipwa mshahara wake kwa muda mrefu.