Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema wizara yake itafanya uchunguzi haraka iwezekanavyo kuhusu uwezo wa mhandisi mkazi na mhandisi ubora wa vifaa wanaosimamia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya kutoka Usesula hadi Komanga mkoani Tabora yenye urefu wa kilomita 108.
Waziri Kamwelwe ametoa kauli hiyo baada ya kukagua barabara hiyo wilayani Sikonge na kutoridhishwa na uwajibikaji wa wahandisi hao hali ambayo imesababisha mkandarasi anayejenga barabara hiyo kupeleka mapipa 3,770 ya lami katika eneo la ujenzi ilhali ubora wake haujathibitishwa.
Amesema haridhishwi na uwezo wa makandarasi wazawa wanaosimamia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya kutoka Usesula hadi Komanga mkoani Tabora yenye urefu wa Kilomita 108.
Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (Afdb) inatumia zaidi ya shilingi Bilioni 158.8 kujenga barabara hiyo.
