Wazee washerehekea siku yao

0
159

Wazee nchini leo wanaungana na wenzao wa mataifa mbalimbali kusherehekea siku ya Kimataifa ya Wazee inayoadhimishwa Oktoba Mosi ya kila mwaka.
 
Katika kuadhimisha siku hiyo, Wazee katika maeneo mbalimbali wamekuwa wakikutana na kujadili mambo yanayowahusu.
 
Taasisi mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya Wazee nazo hutumia siku ya Kimataifa ya Wazee kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili Wazee na kuzitafutia ufumbuzi.
 
Kauli mbiu ya kitaifa ya siku ya Kimataifa ya Wazee kwa mwaka huu ni Matumizi Sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa Rika Zote.