Wazee waomba kuboreshewa huduma za afya

0
149

Wazee wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwaboreshea huduma za afya kwa kuwa katika baadhi ya maeneo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa.

Ombi hilo limetolewa wilayani Rungwe na Mzee
Wille Mwaipopo kwa niaba ya wenzake, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wazee.

Kwa mujibu wa Baraza la Wazee wilayani Rungwe, zaidi ya Wazee elfu 24 wametambuliwa wilayani humo huku wakikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja kutopata huduma stahiki za afya.