Wazee wakumbushwa kufanya mazoezi kuimarisha afya

0
397

Wazee wamekumbushwa kufanya mazoezi ya mwili ili kuimarisha afya ya mwili na kupata tiba afya ya akili na saiokolojia, badala kutegemea kutumia dawa pindi wanapojiona wadhaifu.

Hayo yamesemwa na Shehe wa mkao wa Arusha, Shabaan Juma wakati wa Bonanza lilioandaliwa kwa ajili ya washiriki wa mafunzo yaliyokuwa yakitolewa kwa maafisa ustawi wa jamii, wahudumu wa afya na azaki zinazotoa huduma ya afya ya jamii mkoani Arusha, mafunzo yaliyoandaliwa na taasisi ya PHEDES Tanzania.

Amesema mwili ukifanyishwa mazoezi mara kwa mara unaimarika na kuwa na afya nzuri ya akili hata kama mtu ni mzee, hivyo ni muhimu kufanya mazoezi badala ya kutumia dawa pindi anapojisikia maumivu ya mwili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya PHEDES Tanzania John Ambrose amewashauri maafisa ustawi wa jamii, wahudumu wa afya na azaki zinazotoa huduma ya afya ya jamii kutoa huduma ya afya ya akili na saiokolojia kwa Watanzania wengi zaidi, ili watenge muda wa mazoezi na hivyo kuiweka vizuri miili yao kiafya.

Taasisi ya PHEDES Tanzania kwa kushirikana na AMREF wameendesha mafunzo ya siku tano mkoani Arusha kwa maafisa ustawi wa jamii, wahudumu wa afya na azaki zianazotoa huduma ya afya ya jamii, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutoa huduma ya afya ya akili na saiokolojia kwa jamii.