Wazee, Viongozi Wa Dini Na Wana Siasa Arumeru, Watoa Azimio La Kumpongeza Mhe Rais Magufuli Kwa Kazi Nzuri

0
143

Makundi ya wazee wa mila, viongozi wa Dini pamoja na Wanasiasa Wilayni Arumeru Mkoani Arusha,  wamepitisha Azimio la pamoja kupongeza kazi nzuri zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akisisitiza Jambo wakati wa kongamano la wazee wa wilaya hiyo lililofanyika kwa lengo la kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya kuwatumikia watanzania. 

Wakizungumza wakati wa Kongamano la wazee la wilaya ya Arumeru  Viongozi hao kutoka Makundi mbalimbali wamesema kazi zilizofanywa na Mhe Rais,Dkt. Magufuli kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani hazina kipimo ambapo katika sekta ya Elimu Serikali inatoa Zaidi ya Bilioni 23 katika mpango wa elimu bure na  wilaya ya Arumeru inapata wastani wa shilingi milioni 600 kwa mwezi.

Pamoja na Elimu Serikali ya awamu ya Tano katika sekta ya afya inaendelea kujenga mamia ya vituo vya afya kwa wilaya ya Arumeru ambapo mpaka sasa serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya afya vya Usa river , Nduruma, Mbuyuni kata ya oljoro pamoja na kituo cha afya cha manyire ambacho kimejengwa kwa ubia kati ya serikali ya Tanzania na Japan ambapo kwa sasa vituo vyote vinafanya kazi.

Wazee hao wamesema katika sekta ya afya kwa sasa wilaya inapata wastani wa shilingi bilioni 1 kwa ajili ya dawa na vifaa tiba kila mwaka ambapo katika halmashauri ya Meru serikali inatoa zaidi ya milioni 500 pamoja na Halmashauri ya Arusha serikali inatoa milioni 500 pia katika madawa na vifaa tiba.

Katika tukio lingine la kufurahisha wazee hao wamesema katika sekta ya maji serikali imezindua mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 520 ambapo katika mradi huo jumla ya kata 14 zitanufaika na mradi huo wa maji sambasamba na mradi mwingine wa kuondoa madini ya fluoride kwenye maji ambapo jumla ya shilingi bilioni 8 zimetolewa kwa ajili ya kugharamia mradi huo utakaosaidia kaya zaidi ya elfu 50 kupata maji safi na salama

Wakihitimisha kongamano hilo wazee wamemshukuru Mhe Rais Magufuli kwa kuwajengea barabara kubwa za lami ya njia nne ya sakina tengeru, pamoja na barabara ya By Pass tengeru mpaka ngaramtoni ambazo zimegharimu zaidi ya bilioni 360 ambazo kwa sasa zinatumika.

Wazee wa Arumeru kwa sasa wameingizwa kwenye mpango wa kupewa matibabu bure kupitia mpango wa wilaya kupitia halmashauri kutoa matibabu bure kwa wazee.