Wazazi wasiopeleka watoto Shule Kuadhibiwa

0
160

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka ametoa siku nne hadi Ijumaa, watoto wote wanaopaswa kuwa shule waripoti shule, vinginevyo kutakuwa na adhabu kali kwa wazazi.

Mtaka ameyasema hayo alipokuwa akikagua hali ya kuripoti wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 ambapo wakuu wa wilaya wametakiwa kuwakamata wazazi hao kwa kutumia askari wa mgambo na kuwawajibisha kwa kufanya usafi maeneo ya umma yakiwemo hospitali.

Aidha, amekemea suala la utoro kwa wanafunzi ambapo wakuu wa shule wametakiwa kutumia miongozo ya elimu kuwapa adhabu ili kukomesha utoro na kujenga nidhamu.