Wazazi wakumbushwa wajibu wao kwa watoto

0
172

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwa mstari mbele katika malezi ya watoto na vijana kulingana maadili ya Mtanzania.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro, wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi Kiuma.

Mtariro ameongeza kuwa Taifa linapaswa kusonga mbele likiwa salama kwa kuwalinda watoto na vijana wasiweze kuiga tabia za mataifa yaliyoporomoka kimaadili.

“Wazazi wakiacha kutekeleza wajibu wao kwa watoto hatutaliokoa Taifa, na kama Yesu Kristo alibeba msalaba wake mpaka mwisho kumkomboa mwanadamu iweje wazazi washindwe kusimama kidete kwa ajili ya malezi bora ya watoto”. amesema Mtatiro

Pamoja na mambo mengine amewakumbusha Wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujiwekea akiba ya chakula, badala kukiuza kabla ya msimu na kusababisha migogoro ya kifamilia.