Wawili wateuliwa kugombea ubunge CCM

0
337

 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imewateua Emanuel Cherehani na Mbarouk Amour Habib kuwa wagombea ubunge katika majimbo ya Ushetu mkoani Shinyanga na Konde mkoa wa Kaskazini Pemba.

Uteuzi huo umefanyika wakati wa kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma,  na kuongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan.

Cherehani ameteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Ushetu kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa.

Kwa upande wake Mbarouk Amour Habib ameteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Konde baada ya aliyekuwa mbunge mteule wa jimbo hilo kujiuzulu.