WAUZAJI WA NYAMA WATUNZE AFYA ZA WALAJI NYAMA

0
427

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof Elisante Ole Gabriel anae shughulikia Mifugo amewataka wauzaji wa nyama katika Sekta ya Mifugo nchini watumie mizani bora nakuacha kutumia magogo ili watunze afya za walaji nyama


Ole Gabriel ameyasema hayo baada yakutembelea banda la Wizara ya Mfugo na Uvuvi katika maonesho ya 43 ya Sabasaba na kuipongeza Wizara ya Mfugo na Uvuvi kwa kushinda tuzo ya banda bora na kuwakikishia kuwa mwakani wataibuka namba moja.


Aidha Prof Ole Gabriel ametoa wito wa kuhamasisha watanzania kula nyama zaidi kwa utaratibu mzuri na kuongeza kuwa Ngozi inavirutubisho mahususi ambavyo vinasaidia mtu asizeeke mapema na inaweza kutengeneza vinyuwaji vikali kama bia.


Akamalizia kwa kutoa shukurani kwa Tasnia ya habari kwa mchango wao katika kufikisha elimu mbalaimbali kuhusu mifugo na uvuvi kwa watanzania.