Wauguzi waadhimisha siku yao leo

0
124

Leo ni siku ya Waugizi duniani ambapo Wauguzi wa mataifa mbalimbali wamekuwa wakitumia siku hiyo kukutana na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu taaluma yao.
 
Kauli mbiu ya siku ya Wauguzi duniani kwa mwaka huu ni Wauguzi ni sauti inayoongoza, wekeza na heshimu haki za watu kwa maboresho ya huduma za afya kwa wote.
 
Kitaifa siku ya Wauguzi duniani inafanyika mkoani Kilimanjaro, ambapo zitatolewa hotuba mbalimbali kuhusu siku hiyo na kuhusu taaluma ya uuguzi pamoja na maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wauguzi hapa nchini.

Siku ya Wauguzi duniani inaadhimishwa Mei 12 kila mwaka ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Florence Nightingale ambaye ndiye muasisi wa siku hiyo na ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwa Wauguzi,  sekta ya afya, alisimama kidete katika kuinua viwango vya uuguzi pamoja kuwaelimisha Wauguzi.

Florence Nightingale  alizaliwa katika mji wa Florence, Italy Mei 12 mwaka 1820 na kufariki dunia Agosti 13 mwaka 1910 huko London nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 90.