Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Anthony Mavunde ametoa rai kwa watendaji kuanzia ngazi ya vijiji,
kutimiza wajibu wao kama watumishi wa serikali kwa kufanya kazi kwa
weledi na si kutanguliza maslahi binafsi kutatua migogoro
inayowakabili wananchi.
Mavunde ametoa rai hiyo mkoani Simiyu katika ufunguzi wa maadhimisho
ya wiki ya msaada wa kisheria yanayofanyika kitaifa Bariadi.
Akizungumza katika ufunguzi huo Mwakilishi wa Wizara ya Katiba na
Sheria Felister Mushi amekiri ongezeko la malalamiko ya wananchi
kuanzia ngazi ya vijiji hadi mkoa na kusema kuna umuhimu wa kuangalia
namna ya kupunguza malalamiko hayo kupitia sheria.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema ni vema masuala ya kisheria yakaingizwa katika mitaala ya masomo ya uraia
kwenye shule za msingi na sekondari ili kuwajengea uwezo wanafunzi
katika jamii inayowazunguka.