Watumishi wapya TBC wapigwa Msasa

0
288

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amewataka watumishi wa shirika hilo kuwa wazalendo na kuwa tayari kuitumikia nchi yao.

Akifungua mafunzo ya utumishi wa umma kwa waajiriwa wapya wa TBC Dkt. Rioba amewataka kutambua umuhimu wa chombo cha habari cha umma katika ujenzi wa Taifa.

Dkt. Rioba amewataka watumishi hao bila ya kujali idara zao kuwa waangalizi wa nchi yao ikiwemo kufanya habari za uchunguzi zitakazoibua ubadhirifu katika miradi ya serikali hususani katika kipindi hiki ambacho nchi imeingia katika uchumi wa kati.

Aidha, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia dhima ya Shirika na miongozo yake.