Watumishi wanaojihusisha na rushwa ya ngono waonywa

0
241

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema kuwa, Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu Watumishi wa umma watakaobainika kujihusisha na rushwa ya ngono katika maeneo yao ya kazi.

Waziri Mkuchika ametoa kauli hiyo mkoani Ruvuma, wakati wa katika kikao kazi na Watumishi wa umma wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, kikao kilichokua na lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Amewaambia Watumishi hao wa umma wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kuwa, rushwa ya ngono inadhalilisha na kushusha hadhi ya utumishi wa umma nchini.