Watumishi Nane Ulanga kufikishwa Mahakamani

0
174

https://www.youtube.com/watch?v=hiu9FqLlqNs&feature=youtu.be

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Watumishi pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kutangaza kuwasimamisha
kazi Watumishi Nane wa halmashauri ya wilaya hiyo na kuagiza wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ubadhilifu wa zaidi ya Shilingi Bilioni Tatu za mapato ya ndani.

Watumishi hao ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ulanga, -Yusuph Semguruka ambaye kwa sasa amehamishiwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Rajabu Siriwa ambaye ni Mweka Hazina, Stanley Nyange, Jonson Mwenyembole, Isack Mwansokope, Said Majaliwa, Charles Steven na Hezron Lopa.