Watumishi 13 wa Halmashauri washushwa vyeo Morogoro

0
1515

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI Selemani Jafo ameziagiza mamlaka za nidhamu kuwavua nyadhifa zao watumishi 13 wa Halmashauri ya Ulanga kwa kuhusika na wizi na  ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mia Tisa.

Waziri Jafo pia ameagiza uongozi wa mkoa wa Morogoro kuhakikisha watumishi wote waliohamishwa kutoka Halmashauri ya Ulanga kwenda Halmashauri nyingine wakiwa na makosa warejeshwe ili kuwezesha vyombo vya dola kufanya kazi yake.

Desemba 27 Mkuu wa mkoa wa Morogoro  Dkt. Kebwe Stephen aliagiza kuitishwa kwa baraza la dharura la Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kujadili taarifa ya Tume iliyoundwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI kuchunguza tuhuma za ubadhirifu wa shilingi Bilioni 2.9 zinazodaiwa kutumika kinyume na utaratibu.