Watumiaji umeme waongezeka nchini

0
159

Idadi ya watumiaji wa nishati ya umeme nchini imeongezeka kutoka asilimia 30 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 85 mwaka huu.
Rais John Magufuli amesema kuongezeka kwa idadi ya watumiaji umeme nchini kumechangiwa na kushuka kwa gharama za kuunganisha nishati hiyo ya umeme.


Akihutubia jijini Dodoma wakati wa kufunga bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli amesema kuwa serikali iliamua kushusha gharaza za kuunganisha umeme kutoka zaidi ya shilingi laki tatu hadi kufikia shilingi elfu 27 hivi sasa kwa maeneo ya vijijini.


Amesema katika kipindi kilichobaki cha uongozi wa awamu ya tano, serikali itahakikisha vijiji ambavyo havijapata hiduma ya umeme vinapata huduma hiyo, ili wakazi wa vijiji hivyo waweze kutumia nishati hiyo katika kujiletea maendeleo.


Rais Magufuli ameongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wa serikali ya awamu ya tano nchi haijawahi kuingia gizani kama ambavyo imewahi kutokea katika miaka ya nyuma, na kwamba s