Watuhumiwa Watatu wa Ujambazi wauawa Kigoma

0
589

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa. huku askari polisi wawili wakijeruhiwa baada ya kutokea kwa majibizano ya risasi katika tukio la ujambazi wilayani Kibondo mkoani Kigoma.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma,- Martin Ottieno amethibitisha kutokea tukio hilo nyumbani kwa mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Sophia Dickson, mkazi wa mtaa wa Kanyamahela ambapo watu watu hao walivamia kwa nia ya kupora fedha inayodaiwa kuwa ni ya kiinua mgongo .

Kwa mujibu wa Kamanda Ottieno, Mama huyo naye amejeruhiwa katika tukio hilo baada ya kupigwa risasi Katika bega lake la kushoto na amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo.

Kuhusu akari wawili waliojeruhiwa, Kamanda Ottieno amesema kuwa mmoja amepata majeraha makubwa kwenye mguu wake wa kushoto na taratibu za kumsafirisha kwa ajili ya matibabu zaidi zinaendelea na mwingine ametibiwa na kuruhusiwa.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wa tukio hilo wanaodaiwa kutoroka na limewaomba wakazi wote wa mkoa huo kutoa ushirikiano ili watuhumiwa hao wa ujambazi waweze kukamatwa.