Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi, wameuwa baada ya kutokea kwa majibizano
ya risasi na askari wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam katika matukio mawili
tofauti.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, – Lazaro Mabosasa amesema kuwa, katika tukio la kwanza watu Wawili wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi wameuawa wakiwa katika harakati za kuvamia SACCOSS ya
Msakuzi kwenye eneo la Mbezi Msakuzi, tukio ambalo Polisi walilidhibiti.
Katika tukio la Pili la majibizano ya risasi, Kamanda Mambosasa amesema kuwa, jeshi hilo la Polisi lilimzidi nguvu Emmanuel Peter anayedaiwa kuwa Jambazi Sugu na ambaye alikua anatafutwa na Jeshi hilo kwa muda mrefu.