Watuhumiwa wa ujambazi wauawa Kigoma

0
507

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa baada ya kutokea kwa majibizano ya risasi na askari wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma,  kwenye pori la Moyowosi lililopo wilayani Kibondo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma, – Martin Ottieno amesema kuwa majibizano hayo ya risasi yamezuka baada ya watuhumiwa hao kujaribu kuwashambulia askari waliokua wakiendelea na operesheni ya kuwasaka wahalifu wanaoteka magari kwenye pori hilo.

Kamanda Ottieno  amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linaendesha  operesheni hiyo kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo vya utekaji wa magari na kwamba hadi sasa limekamata vifaa mbalimbali vilivyoporwa ikiwa ni pamoja na simu za mkononi.