Watu wawili wamepoteza maisha baada ya mkazi mmoja wa jijini Mwanza Fungo Mayala kumuua mpenzi wake Hamida Joseph na kisha naye kujiteketeza kwa moto ndani ya nyumba.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza Muliro Jumanne amesema tukio hilo limetokea katika mtaa wa kisiwani kata ya mhandu jijini mwanza baada ya marehemu Mayala kwenda nyumbani kwa marehemu Hamida na kuanza kumpiga hadi kusababisha kifo chake.
