Watu 700 waugua TB bila kujijua

0
282

Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wizara ya Afya, wamefanya zoezi la upimaji wa ugonjwa wa kifua kikuu katika halmashauri nane kati ya tisa za mkoa huo.

Mratibu wa ugonjwa kifua kikuuu na ukoma mkoani Pwani Dkt. Iden Mpangile amesema katika zoezi hilo, zaidi ya watu 700 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu bila wao kujijua.

Amesema idadi kubwa ya watu waliobainika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu mkoani Pwani ni wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 55 ambao baada ya kugundulika wameanzishiwa matibabu bila malipo.