Watu 11 matatani kwa tuhuma za wizi vifaa vya mradi Katavi

0
371

Watu 11 wakiwemo watumishi 5 wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Katavi kwa tuhuma za hujuma kwenye mradi wa ujenzi wa Majengo matano ya Hospitali ya wilaya ya Mlele.

Mkuu wa wilaya ya Mlele, Rachel Kassanda, ameiambia TBC kuwa hujuma hizo ni WIZI wa vifaa vya Ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 15.9.

KASSANDA ametaja vifaa hivyo ni pamoja na saruji, nyaya, vifaa vya umeme na mabati, na vitu mbalimbali ambavyo walikuwa wanaviiba wakati mradi unaendelea kutekelezwa na kwasasa mradi huo umesimama.

Amesema watumishi wa Halmashauri akiwemo afisa manunuzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele Essau Nele, wameagizwa kulipa fedha hizo kabla ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Mlele, unapita katika changamoto nyingi, baada ya mkandarasi aliyepewa zabuni ya kufyatua matofali ambayo yalikuwa chini ya kiwango

Mwandishi: Hosea Cheyo