Watoto wasisahaulike mapambano ya VVU

0
92
Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima amesema,
mkazo unahitajika katika kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa watoto.

Amesema jitihada pia zinahitaji zaidi kuongeza asilimia ya watoto wanaopata huduma bora za kupambana na VVU na kupunguza vifo.

Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ina jumla ya maambukizi ya VVU milioni 1.7, huku watoto walio na umri wa chini ya miaka 14 wakiwa ni elfu 93 na 5,900 kati yao hufariki dunia kila mwaka kwa kuugua Ukimwi.

Byanyima ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuwa kinara katika kupambana na VVU na Ukimwi na kusema jitihada za kupambana na virusi hivyo kwa watu wazima zinaonekana kuzaa matunda kwa zaidi ya asilimia 80 huku watoto wakisahaulika kwani bado ni asilimia 60.

Aidha, amegusia matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa watoto wakati wa kuzaliwa.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameeleza kuwa hadi kufikia hii leo asilimia 98.3 ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wamepatiwa dawa za kufubaza virusi hivyo.