Wateule wa JPM ruksa kujaribu uongozi kwingine

0
250

Rais John Magufuli amesema kuwa Mteule wake yeyote anayetaka kuachia wadhifa wake alionao sasa  na kwenda kugombea nafasi nyingine, ruhusa ipo wazi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni, katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino.

Amesema kuwa katika siku za hivi karibuni ametoa ruhusa nyingi kwa viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na makatibu tawala wa mikoa na wilaya ambao wameamua kuachia nyadhifa zao ili kwenda kujaribu uongozi katika maeneo mengine.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa amekuwa akitoa ruhusa za aina hiyo haraka sana, hivyo yeyote anayehitaji ruhusa hiyo milango ipo wazi.