Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa ubadhirifu na ufujaji wa fedha ambao umesababisha halmashauri hiyo kupoteza kiasi kikubwa mapato.
Zainabu ametoa agizo hilo mjini wakati wa kikao kazi kilichoitishwa
mahususi kwa ajili ya kujadili sababu za kuporomoka kwa makusanyo
katika halmashauri hiyo kutoka shilingi bilioni 1.4 mwaka 2016 hadi
kufikia shilingi milioni 400 mwaka huu.
Kikao kazi baina ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa na
watendaji wa halmashauri hiyo kujadili tatizo la kushuka kwa
ukusanyaji mapato katika halmashauri hiyo umefanyika mjini Bagamoyo
ambapo pamoja na mambo mengine mkuu huyo wa wilaya amekasirishwa na utendaji mbovu wa baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo
Akizungumza katika kikao hicho Zainabu amesema tatizo la kushuka kwa
mapato katika halmashauiri hiyo kunasababishwa na usimamizi mbovu
katika ukusanyaji wa ushuru katika machimbo ya mchanga na hivyo
kuitaka taasisi ya kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watendaji ambao wamesababisha tatizo
hilo.