Watendaji wa Serikali watakiwa kutumia vizuri fedha za miradi ya maji

0
317

https://www.youtube.com/watch?v=xCAlOFKeC5c&feature=youtu.be

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Watendaji wa Serikali mkoani Singida kutumia vizuri fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku Nne mkoani Singida.

Akiwa katika ziara yake hiyo ya kikazi mkoani Singida, tayari Waziri Mkuu Majaliwa amekagua mradi wa maji katika kijiji cha Kintiku wilaya ya Manyoni.