Watendaji mbalimbali wala kiapo Zanzibar

0
147

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, leo amewaapisha watendaji mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

Miongoni mwa watendaji hao walioapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar ni Mgeni Jeilani Jecha aliyeapishwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Valentine Andrew Katema aliyeapishwa kuwa Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar na Shaheen Fauz Mohammed aliyeapishwa kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali.

Hafla hiyo ya kuwaapisha watendaji mbalimbali wa serikali ya mapinduzi Zanzibar imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmeid Said na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji.