Watu watatu wakazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wameuawa kikatili katika matukio tofauti likiwemo tukio moja la kuuawa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 70 aliyechinjwa shingoni na kichwa kutenganishwa na kiwiliwili kisha maiti yake kunyofolewa viungo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani Wankyo Nyingesa, amesema katika tukio la kwanza mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Pongwe Mugula, alibakwa na kisha kuuw
awa katika kitongoji cha Tabora kilichopo kata ya Msata.
Kamanda Wankyo amesema tukio la pili limetokea eneo la Kitonga wilayani Bagamoyo ambapo mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Fatuma Mohamedi mwenye umri wa miaka 70 ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana na kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili.
Amesema mauaji hayo yanahusishwa na imani za kishirikina.
Katika tukio jingine kamanda Wankyo amsema mkulima mmoja mkazi wa Kijiji cha Kwang’andu kilichopo kata ya Mbwewe ameuawa kwa kuchomwa na mkuki na wafugaji waliomvamia akiwa shambani kwake.
Kamanda amesema jeshi la polisi katika mkoa huo linaendesha msako mkali kuwakamata wote waliohusika na mauaji hao.
Katika tukio jingine jeshi hilo loinamshikilia mkazi moja wa mtaa wa Kibondeni mjini Kibaha kwa tuhuma za kukutwa na sare za jeshi la polisi jozi mbili ,mkanda wa polisi mmoja, pamoja na jozi tatu za viatu vya jeshi..
Kamanda Wankyo amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa hatua zaidi.