Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watumishi watatu wa shule ya Sekondari ya Kisomachi iliyopo kata Vunjo Mashariki wilaya ya Moshi
akiwemo Mkuu wa shule hiyo, kwa tuhuma za kusababisha vifo vya Wanafunzi wawili wa kidato cha nne katika shule hiyo.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema, tukio hilo limetokea baada ya Wanafunzi hao kuingia ndani ya tenki linalotumika
kuhifadhia maharage kwa nia ya kutoa maharage baada ya sehemu ya chini inayotumika siku zote kutolea maharage kuziba.
Kamanda Maigwa amewataja Wanafunzi waliofariki dunia kuwa ni Edson Mosha na Godwin John ambapo amebainisha chanzo cha tukio hilo ni Wanafunzi hao kukosa hewa na baada ya kutolewa walikimbizwa kituo cha afya Kirua Vunjo ambapo ilibainika wamekwishafariki dunia.
Miili ya Wanafunzi hao imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Mawenzi kwa uchunguzi zaidi.