Watanzania watakiwa kutokua na hofu kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa

0
161

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara amesema uchaguzi wa serikali za Mitaa utakuwa huru na haki na utasimamiwa kwa kuzingatia sheria na katiba ya nchi.

Naibu Waziri Waitara ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibamba,- John Mnyika aliyetaka kufahamu ni kwanini serikali haibadilishi kifungu cha 74(6) sehemu (e) cha sheria ya uchaguzi wa serikali za Mitaa na kuipa Mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia uchaguzi huo badala ya TAMISEMI.