Watanzania watakiwa kutobaguana

0
552

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Fredrick Shoo ametoa wito kwa Watanzania wote kutenda mambo mema na kwa viongozi kutotumia vibaya madaraka yao kuwanyanyasa wengine.

Askofu Shoo ametoa wito huo katika Kanisa la KKKT Moshi Mjini,  wakati wa Ibada ya kumuaga Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Marehemu Dkt Reginald Mengi.

Amesema kuwa wakati wa uhai wake Marehemu Mengi hakuwa mtu mwenye kiburi na alikua akiwajali na kuwapenda watu wote bila kujali  ukabila wao, Dini wala itikadi za kisiasa.

Askofu Shoo ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kumuenzi Marehemu Mengi kwa kuzidisha upendo miongoni mwao na kotobaguana.

Mara baada ya Misa hiyo katika kanisa la KKKT Moshi Mjini, mazishi ya Dkt Mengi yamefanyika kijijini kwake Kisereni, Machame wilayani Hai mkoani  Kilimanjaro.

Waziri Mkuu  Majaliwa ndiye aliyeongoza mazishi ya Dkt Mengi kwa niaba ya Serikali.

Dkt Mengi alifariki dunia Mei Pili mwaka huu huko Dubai.