Watanzania watakiwa kulinda miundombinu inayotangenezwa na serikali

0
635

Watanzania wametakiwa kulinda miundombinu ya Taifa ikiwemo mradi wa reli ya kisasa (SGR) na barabara ambazo Serikali imewekeza fedha nyingi kutengeneza ili kuharakisha maendeleo ya nchi.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samwel Gwamaka wakati alipotembelea Kituo cha Polisi cha Mlandizi mkoani Pwani kujionea gari aina ya fuso lililokamatwa na Jeshi la Polisi likiwa limebeba shehena ya chuma chakavu zenye mchanganyiko wa vyuma vya ujenzi wa mradi wa reli ya SGR.

Dkt. Gwamaka ameongeza kuwa ni vyema jamii itambue kazi kubwa inayofanywa na serikali kwenye miundombinu ambayo ndiyo chachu ya ukuaji wa uchumi kwa maslahi ya Watanzania wote.

Aidha, amewataka wananchi kuwafichua watu wanaohujumu miundombinu hiyo ili wachukuliwe hatua za kisheria kama sehemu ya kulinda rasilimali za Taifa.