Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, – Padre Alister Makubi ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwachagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
Padre Makubi ametoa wito huo wakati wa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka āCā iliyofanyika katika Kanisa hilo na kuhudhuriwa na Rais John Magufuli, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa pamoja Waumini mbalimbali wa Kanisa Katoliki.
