Watanzania wanufaika ujenzi MV Mwanza

0
124

Meli ya MV Mwanza ‘Hapa Kazi Tu’ imeshushwa kwenye maji katika Bandari ya Mwanza Kusini, ujenzi wake ukiwa umefikia 82%.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamissi ujenzi wa meli hiyo ulianza Januari 2019 ukitoa ajira kwa Watanzania.

MV Mwanza ina urefu wa mita 92.6 na kimo cha mita 20 ambapo gharama za ujenzi ni TZS bilioni 109.1, kati ya hizo mkandarasi amelipwa TZS bilioni 93.8 sawa na asilimia 88 ya malipo.

Meli hiyo itafanya safari kwenye bandari zote kubwa za Ziwa Victoria ambazo zipo ndani na nje ya nchi ambapo itakwenda Bukoba- Tanzania, Musoma-Tanzania, Jinja- Uganda, Port Bell -Uganda na Kisumu- Kenya.

Meli hiyo itatumika kwa ajili ya shughuli za kibiashara, utalii na fungate kusudi watu wote wenye shughuli za shida na raha waweze kusafiri na meli hiyo bila ya kuwepo na vikwazo.