Watanzania wanaadhimisha Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa

0
130

Tanzania leo inaadhimisha Kumbukumhu ya Siku ya Mashujaa kuwakumbuka Mashujaa wote waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda Uhuru wa Taifa lao.

Siku hiyo huadhimishwa ifikapo Julai 25 kila mwaka huku ikiambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo Dua na Sala maalum ya kuwaombea Mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea nchi amani .

Pia hufanyika Gwaride maalum kwa ajili ya kuwaenzi Mashujaa.

Huko mkoani Dodoma
Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan, Leo anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mnara wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba, ikiwa ni sehemu ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa.

Rais Samia ndiye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambayo pia
yatafanyika katika mikoa na wilaya zote nchini kwa kufanya shughuli za kijamii kama vile kupanda miti, kufanya usafi wa mazingira ya kijamii na kufanya Kumbukumbu ya Mashujaa kwa mikoa na wilaya ambapo kuna Minara au Makaburi ya Mashujaa.