Serikali imewarejesha nchini watanzania waliokwama India baada ya katizo la safari kufuatia uwepo wa virusi vya Corona.
Baadhi ya wasafiri wameishukuru serikali kwa kufanikisha kurejea nyumbani.
Meneja Huduma za Afya Mipakani Remedius Kakuru amewashauri wagonjwa kujitenga kwa ajili ya kufuatiliwa Afya zao.
Jumla ya watanzania 246 wamerejea na Ndege ya ATCL kutokea nchini India