Watanzania wakumbushwa kuendelea kutunza Amani

0
247

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amewakumbusha Watanzania wote umuhimu kutunza amani iliyopo nchini.

Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti wa Shamsiyat Bakwata Kilumba, uliopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza,
Mufti amesema kuwa, bila amani hakuna shughuli yoyote ya maendeleo inayoweza kufanyika.

Hata hivyo Mufti amefafanua kuwa, mtu kuzungumzia suala la amani isitafsiriwe kwamba anajipendekeza kwa Serikali, kwa kuwa jambo hilo linapaswa kuzungumzwa na kila Mtanzania.