Watanzania waaswa kuheshimu kazi wafanyazo

0
200

Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuheshimu kazi wanazofanya kwa kuwa ndipo heshima na hatima ya mkate wao wa kila siku ulipo pamoja na kufanyakazi kwa maslahi ya Taifa.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha utengenezaji chokaa, Neelkhant Lime Limited kilichopo eneo la Amani, Tanga Mjini katika siku yake ya tatu kwenye ziara ya siku tano mkoani Tanga.

Kiwanda hicho kinachotoa ajira takribani 1,800 za moja kwa moja kwa Watanzania kimezinduliwa leo na makamu wa Rais, na kinazalisha chokaa bora na malighafi nyingine za kiviwanda zinazotumika ndani na nje ya nchi.

Makamu wa Rais pia ametembelea Kiwanda cha Kutengeneza Kadi Janja (Smart Card) zinazotumika kuchapisha leseni za udereva, kadi za benki, vitambulisho vya taifa, kadi za mahotelini n.k. Kiwanda hicho ni cha kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki.