Watano wauawa katika majibizano ya risasi

0
354

Watu watano wanaosadikiwa  kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na askari wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, – Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Dar es salaam, – Lazaro Mambosasa amesema kuwa watu wengine wanne wanaosadikiwa kuwa pia ni majambazi wamekamatwa katika matukio matatu tofauti.

Kamanda Mambosasa amewataka watu wote wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi kuacha mara moja vitendo hivyo kabla hawajakamatwa na vyombo vya dola.

Pia amewaomba Wakazi wote wa jiji la Dar es salaam kushirikiana na jeshi la polisi ili kuwafichua watu wanaofanya vitendo vya uhalifu.