Watalii kutoka Oman watembelea vivutio vya Utalii Mwanza

0
408

Uwepo wa vivutio vingi vya utalii vikiwemo vile vya asili, Hifadhi za Taifa, mapori ya akiba pamoja na kutokuwepo kwa ugonjwa wa corona nchini, ni baadhi ya sababu zinazochangia Tanzania kutembelewa na Watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali.
 
Miongoni mwa Watalii waliowasili nchini katika siku za hivi karibuni ni wale wa kutoka Oman, ambao kwa sasa wapo jijini Mwanza kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii.
 
Wakiwa jijini Mwanza, Watalii hao wameipongeza Serikali kwa namna inavyoendelea kuboresha sekta ya Utalii, hatua inayowavutia Watalii wengi.

Akizungumzia ujio wa Watalii hao, Afisa Utalii  Mwandamizi Kanda ya Ziwa Dayness Kunzugala amewaomba Watalii hao kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha Watalii kutoka nchini mwao kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.