Watakaohama kupisha mgodi kulipwa fidia

0
111

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amemuagiza mthamini mkuu wa serikali Evelyne Mugasha kukamilisha uthaminishaji fidia kwenye eneo la mradi wa mgodi wa Nyanzaga uliopo Sengerema mkoani Mwanza, baada ya wananchi wa eneo hilo kuelewa taratibu za fidia kwenye eneo hilo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sota wilayani Sengerema wakati wa kufuatilia zoezi la kuwahamisha watu na makazi kwenye mgodi wa Nyazaga Dkt. Mabula amesema uamuzi wa serikali katika kulipa fidia ya kuwahamisha wananchi wa   eneo hilo umezingatia taratibu zote za kisheria zikiwemo za kimataifa na hakuna mtu atakayepunjwa au kukopwa.