Wataalamu waeleza sababu ya Sokwe kupungua Afrika

0
428

Na: Abdulafu Said

KIGOMA: Idadi ya sokwe katika bara la Afrika imeendelea kupungua kutokana na kukithiri kwa uharibifu wa mazingira unaotokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu katika hifadhi na maeneo jirani wanapoishi wanyama hao.

Hayo yamebainishwa na Mtafiti wa Sokwe Duniani, Jean Goodle wakati akizindua programu ya kupanda miti ili kutunza mazingira mkoani Kigoma, na kusema kuwa mpaka sasa idadi hiyo imepungua kutoka sokwe milioni moja hadi laki tatu.

Historia inaonesha kuwa katika miaka ya 60 Sokwe walipatikana katika maeneo mengi lakini kwa sasa masikani yao yanatumika na binadamu kwa makazi na kilimo jambo lililofanya wakose mahali kwa kuishi.

Mbaya zaidi hata katika maeneo yaliohifadhiwa kwaajili ya makazi yao kama vile Gombe na Mahare napo kunakabiliwa na uharibifu wa mazingira ambapo athari yake haikuishia kwa Sokwe pekee bali kuzalisha maafa ya maporomoko ya udongo kwa wakazi wanaoishi vijiji jirani na milima ya Gombe ambapo mwaka 2001 watu walifariki dunia baada sehemu ya mlima kuporomoka na kufukia nyumba zaidi ya 40 katika Kijiji cha Mtanga.

Mkazi wa Kijiji cha Mtanga akishiriki zoezi la upandaji miti kando ya Mlima Gombe.

Katika kubabiliana na uharibifu huo asasi isiyo ya kiserikali ya Jean Goodle imeanzisha programu maalum ya upandaji miti na kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi wanaoishi jirani na hifadhi ili kulinda uhai wa viumbe waliopo

Farida Abdallah, mkazi wa Kijiji cha Mwangongo akitayarisha mti kwa ajili ya kuupanda kando ya Mlima Gombe

Kwa upande wake afisa misitu wa halmashauri ya Kigoma vijijini ambapo hifadhi hiyo inapatikana amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo jirani kuendeleza juhudi hizo ili kulinda uhai wa miti inayopandwa