Wasichana wang’ara matokeo ya kidato cha nne

0
168

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo Januari 15, 2021 limetangaza matokeo ya kidato cha nne, QT, kidato cha pili na darasa la nne na kutoa orodha ya watahiniwa kumi bora kitaifa inayoongozwa na wasichana.

Nafasi nane kati ya kumi zimeshikwa na wasichana, huku wavulana wakicjitokeza katika nafasi ya nane na tisa.

Shule ya St. Francis iliyopo Mbeya imeibuka kinara kwa kutoa wanafunzi saba kati ya kumi bora kitaifa ambapo katika nafasi ya kwanza hadi ya tano wahitimu wa shule hiyo ndio vinara.

Shule ya Bright future Girls iliyopo Dar es Salaam imetoa mwanafunzi mmoja nafasi ya sita, Feza Boys’ iliyopo Dar es Salaam ikiwa na mwanafunzi mmoja nafasi ya nane na nafasi ya tisa ikienda kwa shule ya Ilboru iliyopo Arusha.

Japo wasichana wanaongoza katika nafasi za juu kitaifa, wavulana wanaongoza kwa ufaulu mkubwa zaidi.

Kati ya wanafunzi 483,820 waliofanya mtihani wa kidato cha nne, wanafunzi 422,388 wamefaulu, sawa na 87%. Wasichana wakiwa 218,174 sawa na 85.77% na wavulana waliofaulu ni 204,214 sawa na asilimia 89.00%

Ufaulu wa matokeo ya mwaka 2021 umeongezeka kutoka 85.84% mwaka 2020.