Shirikisho la Vyama vya Waajiri kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), limeshauri Mifuko ya Hifadhi za Jamii itambulike kwa nchi zote Wanachama wa Jumuiya hiyo.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa Makatibu Wakuu wa wizara za Kazi na Ajira kutoka nchi za SADC, Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri nchini (ATE) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Waajiri kwa nchi za SADC Dkt Agrey Mulimuka amesema kuwa, hatua hiyo itawawezesha Wafanyakazi kuvuka mipaka na kwenda kufanyakazi kwenye nchi yoyote ya SADC bila hofu.

Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira kutoka Tanzania, – Andrew Masawe amesema kuwa bado changamoto ya upungufu wa ajira ni kubwa sio tu kwa nchi za SADC bali kwa duniani nzima, hivyo ametaka kuwepo kwa mikakati ya pamoja yenye lengo la kukabiliana na changamoto hiyo.
