Wasanii waiomba Serikali kutatua changamoto zao

0
151

Wasanii nchini wameiomba Serikali kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali, ambazo wamekua wakikutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Akisoma risala ya Wasanii kwa niaba ya wenzake, Msanii Yvonne cherryl ayetambulika kwa jina la kisanii kama Monalisa amesema kuwa, changamoto zao zikishughulikiwa, wataweza kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

Katika risala yao, Wasanii hao wameomba kuwepo kwa Watendaji wa kutosha wa Taasisi zote zinazohusika na Wasanii, Watendaji ambao watasambazwa katika maeneo yote nchini ili waweze kushughulikia mambo yao.

Pia wametaka kuwepo kwa usimamizi mzuri wa kazi za Sanaa, ili Wasanii waweze kufanya kazi zao vizuri zaidi na kujiongezea kipato chao pamoja na kuchangia katika pato la Taifa.

Wasanii hao wametoa ombi hilo jijini Dar es salaam, wakati wa Tamasha la Sanaa la Mwalimu Nyerere, tamasha lililohudhuriwa na Wasanii mbalimbali.